Harmonize Awajia juu Mashabiki wanaomponda kuwa anamuiga Diamond

Shutuma kuwa amekuwa akimuiga bosi wake Diamond, zimemchosha Harmonize na sasa ameamua kujibu. 

Baada ya video ya wimbo Inde alioshirikishwa na Dully Sykes kutoka, mashabiki ndio wamezidi kuendelea kusisitiza kuwa msanii huyo anamuiga kwa kiasi kikubwa Diamond.
 

Harmonize ambaye mara nyingi amekuwa akisisitiza kuwa ndivyo yeye alivyo na yeye sasa ameonekana kuchoshwa na malalamiko ya mashabiki hao ambapo amejikuta akiandika ujumbe wenye utata kwenye Instagram:

Mhhh copy! copy! copy!….. mwisho wa siku hata ukinya utaambiwa kunya kama wewe usimcopy@diamondplatnumz ebwana mzee#simbaa video ijayo wacha nianze kuvaa Dera maana nguo zote ushazivaa ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ#INDE in my BIO though๐Ÿ˜Š
Harmonize Awajia juu Mashabiki wanaomponda kuwa anamuiga Diamond Harmonize Awajia juu Mashabiki wanaomponda kuwa anamuiga Diamond Reviewed by on 2:33:00 AM Rating: 5